Tunarahisisha biashara ya kupangisha nyumba.
Tumejikita katika kupangisha nyumba na ku-manage mchakato mzima wa kupanga nyumba.
Kuhusu Pangisha
Tuna huduma kuu mbili: moja ni ya udalali (kutafutia wateja nyumba za kupanga), na ya pili ni program ya kutunza kumbukumbu za mchakato mzima wa kupangisha nyumba — ikizingatia mmiliki wa nyumba, nyumba yenyewe, mpangaji, mkataba wa nyumba pamoja na makusanyo ya kodi.
Maono
Kila mwenye nyumba Tanzania kusimamia mali zake kwa ujasiri na uhakika — akiwa na nguvu kamili ya kujiendesha mwenyewe.
Dhamira
Kuwawezesha wamiliki na wasimamizi wa mali kwa mfumo rahisi na salama, tukifundisha kwa kuzingatia uelewa wa mteja na subira, na kubaki washirika wao tukisikiliza na kuboresha bila kukoma.
Malengo
Ifike muda jamii ya Kitanzania ihame kutoka kwenye daftari (counter book) na faili za Excel katika biashara ya kupangisha nyumba, na badala yake itumie program yetu ya Pangisha.
Gharama
Gharama zetu zinaanzia 10,000/= Tshs kwa mwezi na zinategemea idadi ya nyumba unazozisimamia. Chagua mpango unaokufaa — bila mkataba wa muda mrefu.
- Unit 1 – 10
- SMS 100 kwa miezi 6 – 12
- Viambatisho hadi 5MB
- Bei flat (haibadiliki)
Unit 1 inahesabika kwa mpangaji mmoja (1).
- Unit 11 na zaidi
- SMS kulingana na idadi
- Viambatisho 10MB na zaidi
- Bei inakua sambamba na biashara
Wateja wakubwa (Unit 100+) wanaweza kupata punguzo — wasiliana nasi.
Wasiliana Nasi
Fika Ofisini
Ofisi yetu iko:
12 Mori St, Sinza A,
Dar es Salaam, Tanzania
Karibu wakati wowote wa kazi.
Saa za Kazi
Jumatatu – Ijumaa:
Saa 3:00 asubuhi – 11:00 jioni
Jumamosi:
Saa 3:00 asubuhi – 8:00 mchana
Uko tayari kuanza?
Jaribu mfumo mwenyewe bila malipo, au wasiliana nasi — tutakusaidia haraka.