Mkataba wa Kupangisha Nyumba — E-Lease (Demo)
Picha ya Mpangishaji
|
Mkataba wa Kupangisha Nyumba
Pangisha Company |
Picha ya Mpangaji
|
Mkataba wa kupangisha nyumba kati ya Ndugu Juma Mohamed Ally na Ndugu Amina Rashidi Hassan.
Katika rejea ya maandishi ya mkataba huu, Ndugu Juma Mohamed Ally ni mwenye nyumba na MPANGISHAJI. Ndugu Amina Rashidi Hassan, ambaye picha yake imebandikwa juu kulia, ni MPANGAJI.
Katika mkataba huu MPANGISHAJI amekubali kupangisha nyumba yake iliyopo Msasani, Kinondoni, Dar es Salaam kwa muda wa miezi 12 tu, kuanzia tarehe 01-Mei-2026 mpaka tarehe 30-Aprili-2027, kwa kiasi cha kodi ya 3,600,000 Tshs (kodi ya mwezi mmoja ni 300,000 Tshs) bila mapunguzo yeyote.
Makubaliano ya mkataba huu ni kama yafuatayo:
- Mpangaji atalipa kodi ya nyumba mapema siku ya kwanza ya kila mwezi bila kukumbushwa na mpangishaji.
- Mpangaji hatatoa watu wengine kukaa ndani ya nyumba hiyo bila idhini ya maandishi ya mpangishaji.
- Mpangaji atatunza usafi wa nyumba na mazingira yake wakati wote wa upangaji.
- Mpangaji hatafanya marekebisho, ujenzi, au mabadiliko yoyote ya nyumba bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mpangishaji.
- Mpangaji ataripoti uharibifu wowote wa nyumba kwa mpangishaji ndani ya siku mbili (2) baada ya kuugundua.
- Mpangaji hatatumia nyumba kwa shughuli yoyote ya biashara isipokuwa kwa makazi ya kawaida ya familia.
- Mpangaji atamuachia mpangishaji nyumba katika hali nzuri sawa na ilivyokuwa wakati wa kuingia, ikiwemo usafi wa kina na kurejesha vitu vyote vilivyopewa.
- Ikitokea mpangaji atataka kumaliza mkataba kabla ya muda wake, ni lazima atoe notisi ya maandishi ya miezi miwili (2) kwa mpangishaji.
- Mpangishaji ana haki ya kutembelea na kukagua nyumba wakati wowote, lakini ni lazima atoe taarifa ya angalau siku moja (1) kabla ya ziara.
- Malipo ya umeme, maji, takataka, na huduma zote za kila siku ni jukumu la mpangaji peke yake.
- Mpangaji hataruhusu wanyama wa aina yoyote ndani ya nyumba bila idhini maalum ya maandishi ya mpangishaji.
- Kama mpangaji atakosea kulipa kodi kwa muda zaidi ya siku kumi na nne (14), mpangishaji ana haki ya kuchukua hatua za kisheria za kumwondoa.
NB: Kila upande umesoma na kukubaliana na masharti ya mkataba huu.
Kwa kutekeleza masharti ya mkataba huu pande zote mbili wameweka sahihi zao kama ifuatavyo:
MPANGISHAJI
| Jina Kamili | Tarehe | Namba ya Simu | Sahihi |
|---|---|---|---|
| Juma Mohamed Ally | +255 712 345 678 | Sahihi |
MPANGAJI
| Jina Kamili | Tarehe | Namba ya Simu | Sahihi |
|---|---|---|---|
| Amina Rashidi Hassan | +255 754 321 987 | Sahihi |
SHAHIDI WA MPANGISHAJI
| Jina Kamili | Tarehe | Namba ya Simu | Sahihi |
|---|---|---|---|
| Sahihi |
SHAHIDI WA MPANGAJI
| Jina Kamili | Tarehe | Namba ya Simu | Sahihi |
|---|---|---|---|
| Sahihi |
© 2026 Pangisha Company — msaada@pangisha.co.tz — +255 657 999 441
Weka Sahihi Yako
Pumzisha Daftari, file la Excel au Counterbook
Tuambie una nyumba (units) ngapi unapangisha vilevile ungependa upate kipi cha ziada kupitia program yetu ya Pangisha. Tuna imani utafurahishwa na Program yetu kwa aslimia mia (100%)
"Kuza biashara yako ya kupangisha nyumba kwa kutumia progran ya kidijitali ya Pangisha, ni njia bora na rahisi ya kuendesha biashara ya kupangisha nyumba kati ya mwenye nyumba na mpangaji."
"Kulingana na nyumba nyingi nilizonazo, Program ya Pangisha imenisaidia ku-keep track ya wateja wapi wamepitiliza muda wa kukaa kwenye nyumba nilizowapangisha, hivyo sijawahi kusahau tena, Program inakumbusha kila mara na inaniwezesha kuwakumbusha wapangaji wangu."
"Nimekuwa nikipitia kipindi kigumu kupata taarifa za wapangaji wangu vilevile taarifa za mikataba ya pango kulingana na idadi kubwa ya nyumba zangu za kupangisha. Nafurahia sana urahisi wa kupata taarifa kuhusu nyumba zangu za kupangisha na kuhusu wateja wangu kila ninapozihitaji."
Picha ya Mpangishaji
Picha ya Mpangaji