MASWALI
Maswali yanayoulizwa mara kwa mara.
Mali yako, mkononi mwako. Majibu ya haraka kwa kila unachotaka kujua kuhusu Pangisha.
Bei na Malipo
01Bei inategemea idadi ya wapangaji wako. Ukiwa na wapangaji 1 hadi 10, unalipa Shilingi 120,000 kwa mwaka. Ukiwa na zaidi ya wapangaji 10, unalipa Shilingi 1,000 kwa kila mpangaji kwa mwezi.
Ndiyo. Unaweza kulipia kwa mkupuo wa miezi 6 au mwaka mzima (miezi 12) — chagua kinachokufaa.
Jinsi Mfumo Unavyofanya Kazi
02Pangisha ni mfumo unaokusaidia kusimamia wapangaji wako wote mahali pamoja. Unaona mikataba yote, malipo, nani kalipa na nani hajalipa, na chumba kipi kina mpangaji au kipi kipo wazi — yote mtandaoni, bila daftari wala makaratasi.
Mfumo hutuma ujumbe wa SMS kiotomatiki kuwakumbusha wapangaji kabla kodi haijaisha — siku 30 kabla, siku 7 kabla, na siku ya mwisho. Wewe mmiliki pia hupokea taarifa kila mkataba unapoelekea kuisha.
Hapana. Pangisha haishiki wala kukusanya pesa za wapangaji. Kazi yake ni kutunza kumbukumbu na kutuma vikumbusho kwako na kwa wapangaji wako.
Hakuna tatizo. Mfumo hutuma SMS za kawaida zinazofika kwenye simu yoyote. Wapangaji hawahitaji simu za kisasa wala intaneti.
Matumizi ya Mfumo
03Kwa sasa Pangisha inatumika kupitia tovuti (website) ukiwa na intaneti. Programu ya simu (app) inatengenezwa na itapatikana hivi karibuni.
Wewe mmiliki huingia kwa jina lako la mtumiaji na neno la siri. Ukipenda, unaweza kumpa mtu mwingine — kama meneja au mwanafamilia — ruhusa ya kuendesha akaunti kwa niaba yako.
Inawezekana kabisa. Tunasajili vyumba vyako vyote bila kujali vipo maeneo gani, na kila nyumba inaonekana peke yake ikiwa na vyumba vyake.
Ndiyo, muda wowote. Vyumba vipya vinaongezwa kwenye akaunti yako ile ile, na unalipia tu kwa vile ulivyoongeza.
Ndiyo. Usalama wa taarifa zako umezingatiwa kikamilifu na taarifa zako zinahifadhiwa kwa usalama.
Kuhusu Pangisha
04Tunawahudumia wamiliki wa nyumba na majengo wanaopangisha — tukiwasaidia kusimamia wapangaji, mikataba na malipo.
Aina zote — nyumba za kupanga, hosteli, maghala (goddown), vyumba single na double. Kila mpangaji huhesabika kama mmoja.
Ofisi yetu kuu ipo Dar es Salaam, lakini tunahudumia wateja nchi nzima.
Ni rahisi: tunakufungulia akaunti na kukuelekeza jinsi ya kuitumia. Unaweza pia kuomba demo ya bure kupitia Google Meet au Zoom kabla ya kuanza.