Pangisha Company
12 Mori St, Sinza A, Dar es Salaam, Tanzania
Tel: +255 657 999 441 / +255 612 73 71 72
Barua pepe: msaada@pangisha.co.tz
Picha ya Mpangaji
Mkataba wa kupangisha nyumba kati ya Ndugu Juma Mohamed Ally na Ndugu Amina Rashidi Hassan.
Katika rejea ya maandishi ya mkataba huu, Ndugu Juma Mohamed Ally ni mwenye nyumba na MPANGISHAJI. Ndugu Amina Rashidi Hassan, ambaye picha yake imebandikwa juu kulia, ni MPANGAJI.
Katika mkataba huu MPANGISHAJI amekubali kupangisha nyumba yake iliyopo Msasani, Kinondoni, Dar es Salaam kwa muda wa miezi 12 tu, kuanzia tarehe 01-Mei-2026 mpaka tarehe 30-Aprili-2027, kwa kiasi cha kodi ya 3,600,000 Tshs (kodi ya mwezi mmoja ni 300,000 Tshs) bila mapunguzo yeyote.
Makubaliano ya mkataba huu ni kama yafuatayo:
Mpangaji atalipa kodi ya nyumba mapema siku ya kwanza ya kila mwezi bila kukumbushwa na mpangishaji.
Mpangaji hatatoa watu wengine kukaa ndani ya nyumba hiyo bila idhini ya maandishi ya mpangishaji.
Mpangaji atatunza usafi wa nyumba na mazingira yake wakati wote wa upangaji.
Mpangaji hatafanya marekebisho, ujenzi, au mabadiliko yoyote ya nyumba bila ruhusa ya maandishi kutoka kwa mpangishaji.
Mpangaji ataripoti uharibifu wowote wa nyumba kwa mpangishaji ndani ya siku mbili (2) baada ya kuugundua.
Mpangaji hatatumia nyumba kwa shughuli yoyote ya biashara isipokuwa kwa makazi ya kawaida ya familia.
Mpangaji atamuachia mpangishaji nyumba katika hali nzuri sawa na ilivyokuwa wakati wa kuingia, ikiwemo usafi wa kina na kurejesha vitu vyote vilivyopewa.
Ikitokea mpangaji atataka kumaliza mkataba kabla ya muda wake, ni lazima atoe notisi ya maandishi ya miezi miwili (2) kwa mpangishaji.
Mpangishaji ana haki ya kutembelea na kukagua nyumba wakati wowote, lakini ni lazima atoe taarifa ya angalau siku moja (1) kabla ya ziara.
Malipo ya umeme, maji, takataka, na huduma zote za kila siku ni jukumu la mpangaji peke yake.
Mpangaji hataruhusu wanyama wa aina yoyote ndani ya nyumba bila idhini maalum ya maandishi ya mpangishaji.
Kama mpangaji atakosea kulipa kodi kwa muda zaidi ya siku kumi na nne (14), mpangishaji ana haki ya kuchukua hatua za kisheria za kumwondoa.
NB: Kila upande umesoma na kukubaliana na masharti ya mkataba huu.
Kwa kutekeleza masharti ya mkataba huu pande zote mbili wameweka sahihi zao kama ifuatavyo:
Tunapatikana kwa mawasiliano kupitia barua pepe na namba za simu zilizoainishwa.
Vilevile kupitia kifungo chekundu (Red Button) kwenu Menu ya juu unaweza kutueleza mahitaji yako na sisi
tunawasiliana na wewe ndani ya masaa ishirini na nne (24).
Fika Ofisini
Ofisi yetu iko: 12 Mori St, Sinza A, Dar es Salaam, Tanzania