logo

Program #1 Tanzania ya Pango

Simamia biashara yako ya nyumba za kupanga, ofisi, na kumbi kidijitali, data zako zitizame ukiwa popote.

 • shape
 • shape
 • shape
hero image
hero image

Faida za Program ya Pangisha

Tumejikita kuhakikisha unasimamia nyumba za kupangisha katika nyanja za kupokea kodi kwa wakati stahiki bila kusahau kwa namna yoyote ile.

MAKUSANYO

Tunakupa Uhakika wa kukusanya kodi zote za Pango kwa wakati kwa kukukumbusha pale mkataba wa mteja unapoisha.

MIKATABA

Ni rahisi kukagua mikataba ya wapangaji wako kufahamu ni mikataba ipi ni ya sasa, ilimaliza muda wake au inayokaribia kuisha muda wake.


DATA

Data zako unaweza kuzitazama popote na wakati wowote kwani zimehifadhiwa katika mtandao wa kidijitali vilevile ziko sehemu salama kabisa.

Yaliyomo

Sifa za Program ya Pangisha

Vipengele muhimu vya programu ya Pangisha vimepangiliwa kulingana na hatua za kuingiza data. Bonyeza kifungo (Button) husika kwa maelezo kuhusu kipengele chake.

Linganisha

Pangisha au Daftari

Muhimu kulinganisha matumizi ya kawaida ya Daftari (Counterbook) au Program ya Pangisha katika kusimamia biashara ya kupangisha nyumba.

 • Imerahisishwa

  Ni rahisi kupata Mkataba au taarifa za mpangaji

  Ni rahisi kupata mkataba fulani au taarifa za mpangaji fulani kupitia program ya Pangisha.

 • Njia Salama

  Data zimehifadhiwa sehemu salama

  Program yetu tumeiwekea kinga madhubuti dhidi ya wiza wa mitandaoni vilevile tunatunza copy ya data zaidi ya hifadhi (storage) moja

 • Makusanyo Sahihi

  Program inakupa namba sahihi ya makusanyo

  Program yetu inafanya mahesabu ya makusanyo sahihi kulingana na taarifa za mikataba na malipo zilizoingizwa tayari. Hakuna kinachosahaulika. Unaweza kutoa ripoti na kukagua mwenyewe nje ya program.

 • Mawasiliano Rahisi

  Uwezo wa kutuma SMS kwa mkupuo

  Ni rahisi kutuma ujumbe kwa njia ya SMS kwa wapangaji wengi kwa wakati mmoja kuwakumbusha kuhusu kodi au dharura ya namna yoyote (mfano matengenezo ya lifti) katika jengo fulani.

 • Ugumu

  Ni ngumu kupata taarifa za mkataba au mpangaji.

  Kwa daftari ni ngumu kutafuta taarifa za mpangaji kwani hujui yuko kurasa gani

 • Si salama

  Daftari kupotea

  Daftari linaweza kupotea au kuharibiwa kwa majanga ya moto au kunyeshewa na mvua hivyo kukosa taarifa sahihi za biashara yako.

 • Kukosa Makusanyo Sahihi

  Ni rahisi kukosea kufanya mahesabu

  Kujumlisha kodi za mkataba mmoja mmoja kwa kutumia Calculator au kwa kutumia kichwa ni rahisi kukosea na kupata jumla isiyo sahihi. Bado unaweza kupata maradhi ya kuumwa kichwa.

 • Ugumu wa Mawasiliano

  Mfano uwezo wa kutuma SMS kwa wapangaji wako wote

  Kwasababu namba za simu ziko kwenye daftari, inachosha kutuma ujumbe kwa mpangaji mmoja mmoja ukizingatia unaweza kuwa wapangaji zaidi ya mia moja, hivyo ufuatiliaji nao ni mgumu.